اخبار

AYA AMBAZO WAMEKOSEA KUZIFAHAMU WATU WA MISIMAMO MIKALI

Umepewa mtihani umma kwa kuwepo kikundi cha watu wachache hapo zamani na hivi sasa ambao kiliufahamu Uislamu ufahamu ulio na makosa wakazitafsiri aya za Qur an kwa tafsiri zisizokuwa sawa kwakuwa walijitosa Katika kuzifanyia tafsiri zisiyo sahihi, haionyeshi tafsiri hizo kuwa katika muundo sahihi wa Qur an wala haitegemezwi katika kanuni za kisheria zilizo sahihi wala haitegemei katika kanuni za lugha ya kiarabu iliyo sawa, ikawa sababu ya kumzulia Mwenyezi Mungu uongo na uzushi  na wakazitolea hukumu aya za Mwenyezi Mungu hukumu iliyo mbali na kupatia, wakidhania kwa ufahamu huu ulio na ugonjwa na wanajifanya Kwamba wao wanashikilia usukani wa dini na wao ndio walinzi na walezi wa sheria, hakika amehadharisha mtume Muhammad ( SAW ) katika hadithi iliyo sahihi ambayo ameweka wazi ndani yake kwamba hao ni watoto wadogo, wapungufu wa akili wanadharau swala zenu pamoja na swala zao na funga zenu pamoja na funga zao wanaisoma Qur an lakini haifiki hata katika koo zao wenye kutiwa kufitiniwa mioyo yao pamoja na nyoyo za watu wanaowafata katika mambo yao wanaruka katika dini kama inavyoruka mshale kutoka katika upinde, Hao ni katika Makhawariji wa zamani na wamezalisha mimea mibaya katika kizazi hiki nao ndio Makhawariji wa zama hizi wamepita njia za watu waliotangulia na wakaondosha bendera ya uislam kwa maneno ya uongo na uzushi na wakaeneza katika ardhi ufisadi na wakaisifu jamii kwa ujinga na wakawahukumu watu wa mataifa yao na hukumu zao kuwa ni ukafiri wakatia dosari sura ya uislamu wakawatumia maadui wa nchi na kuwabebesha silaha kwa ajili kuharibu miji wakawa wanakufurisha watu na kuhalalisha mali zao na vyeo vyao na kuhalalisha kuuliwa aliye ndani ya jamii hiyo, na wala hazikusalimika jamii za kiarabu na kiislam ukiachilia mbali haki za kibinadamukwa hali ambayo umewaka ulimengu mzima moto wa misimamo yao mikali ya ugaidi.

Mtu ambae atakayesoma kwao au kusikiliza hutuba zao au akasoma Makala zao wanazozieneza katika mitandao ya kijaamii haili ya kuwa wanakusudia katika malengo yao kuwabebesha silaha vijana wa kiume na wakike kwa jina la dini, na hali ya kuna dini ipo mbali na matendo yao hayo na mwenye kuzingatia katika kila walicho kieleza lau kingepitisha katika kanuni sahihi na kanuni za kisheria na makusudio yake na kanuni za lugha na mapito yake angekuta maneno yao yanaanguka kabisa na hayana mazingatio lakini wanawadanganya watoto wadodo wadogo na wenye uelewa kwa kuwafata na mambo yanayogusa dini.

Hivi hatuoni kuwa wao wanadai kwamba aya zote zinazozungumzia ahadi  kusamehe na Amani kuwa zimefutwa kwa aya za vita, haya ni madai ya uongo pia hayana hoja thabiti, isipokuwa jambo ambalo wamekubaliana wanachuoni wa zamani na waliofatia  kuanzia zama za maswahaba mpaka leo hii wamekubaliana aya za Ahadi na Msamaha na Amani hazifutwi, na hakika Amani ndio msingi wa kila kitu, ama vita ni jambo ladharura ambalo ameliweka Mwenyezi Mungu kwa waja wake kwa ajili ya kuzuia maadui na kuihami miji na kuipa Amani njia ya kumlingania ALLAH ili awe mlinganiaji na mlinganiwa katika Amani. Na haki ya kujitetea linakubaliwa na kanuni zote za kimchi, sasa utaona kutokana ujinga wao wanashindwa kutofautisha aya za jihadi na mapigano, kwa mfano wao wanachanganya ajya za jihadi na mapigano kwani tafsiri sahihi ni kwamba aya za jihadi ni zenye kukusanya Zaidi kuliko aya za mapigano kwakuwa JIHADI inakuwa kwa kauli au hoja au dalili, sio kwa silaha kama wanavyofahamu hawa wajinga. Anasema Mwenyezi Mungu mtukufu

{ ewe mtume wapatie hoja makafiri na wanafiki na wawekee ugumu hao na mafikio yao ni motoni na hayo ni mafikio mabaya kabisa }

Hakika sio vinginevyo bali hiyo ni amri ya kupambana kwa hoja na mtu ambaye amepinga utume wake katika washirikina wa Maka na wle walioficha Imani zao katika nyoyo zao nao ni wanafiki wa Madina. Na wala haijawahi kunuu historia yoyote kwamba mtume aliwahi kuwapiga wanafiki kabisa, isipokuwa makusudia ya jihadi katika ayah ii ni kubishana kwa hoja na dalili na sio kwa silaha

Ama aya za vita ambazo wamezitafsiri kama zilivyo bil kuchunga kanuni ambazo zimezingatiwa na sharia na wao wakazipandanisha sentensi kimakosa na wakazichelewesha na muundo wake na wakazifanya kuwa zenye kuenea katika kumpiga kila anayeenda kinyume na fikra zao , lau wangezikatia wangeona kuwa ile amri ya vita ni sharia kwa mtu anayetaka kutupiga au anamsaidia mtu anaye tupiga au antaka kututoa katika miji yetu au anataka kuandamana ili atutoe katika miji yetu.  Tusome kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu.

{ wapigeni vita kwa ajili ya ALLAH wale ambao wanakupigeni wala musifanye uadui kwani hakika ya ALLAH hawapendi wafanya uadui }

Zingatia ni vifungu vingapi vipo katika ayah ii ambayo Mwenyezi Mungu ametuarisha kuwapiga wale wanaotupiga .   pia soma kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu.

{ Yoyote atakaye wafanyia uadui nanyi mrudushieni mfano wa alivyokufanyieni }

Kama hivi ndio aya zote zilizobakia katika vita zimekuja kwa ajiliya kujitetea na kuihami miji na kuihafadhi dini kwa hali yoyote. Basi itwalaq hapa ni yenye kudhibitiwa, kama anavyosema Mwenyezi Mungu mtukufu

{ Hawakatazi ALLAH kuwafanyia wema na uadilifu wale wasiowpiga katika dini wa kuwatoa katila dini, Hakika ALLAH anawapenda wenye kufanya uadlifu } na kama anavyosema kuhusu washirikina wa Makka.

{ Ila wale ambao mumeahidiana nao katika msikiti mtukufu wakiwa sawa kwenu nanyi kuweni sawa kwao hakika ALLAH anawapenda wachamungu }  kama anavyosema Mwenyezi Mungu mtukufu

{ Ikiwa wanahitaji Amani wapatie hiyo amani na umtegemee allah}    kama anavyosema Mwenyezi Mungu mtukufu

{ Enyi mlioamini ingieni katika Amani hali ya kuwa ni wote }

Hakuna aya katika uislam inayoamrisha kupigana au kumuua mwanaadamu eti kwa sababu ya kutofautiana itikadi,  kama anavyosema Mwenyezi Mungu mtukufu

{ Lau angetaka mola wako wangeamini watu wote waliopo ardhini, hivi wewe ni mwenye kulazimisha watu kuamini }

{ Lau angetaka mola wako angewafanya wwatu wote kuwa umma mmoja lakini hawaachi kuwa ni wenye kutofautiana, na kwa ajili hiyo allah kawaumba hao } 

Na haikuwa sababu ya kuuwa katika sharia sio ukafiri wa kafiri kwakuwa kafiri wa asili ni mwenye hauwawi kisheria isipokuwa sababu ya kuuliwa ni kutufanyia uadui sisi na sisi kujitetea na uadui wake.

Ajihadhari kijana wa kiislam popote alipo kuchukua tafsiri za watu wa misimamo mikali kuwafata watu wa batwili na kuchukua tafsiri za wajinga,  na atambue kwamba kusamehe katika uislamu ni hukumu yenye kuendelea mpaka siku ya kiama na sharia ya vita ni hukumu yenye kuendelea mpaka siku ya kiyama ameiweka Mwenyezi Mungu kwaajili ya kujihami na kutetea mambo matukufu ya uislam na hata yasiyo ya kiislam, uhakika wa hilo ni kauli yake Mwenyezi Mungu mtukufu

{ Lau kama sio kuwatetea watu ALLAH basi yangevunjwa majumba ya ibada ambapo hujwa jina la ALLAH sana na ALLAH anamnusuru yule anaye mnusuru hakika ALLAH ni mwenye nguvu na mshindi }

Na ashikane kijana na uislam ulio sahihi na sharia zake zilizo tukuka na achukue elimu zao na fahamu zao kutoka katika wanachuni wa wa umma wenye kuaminika ambao yamekusanya macho yao katika kujifunza na kufundisha na kuchambua vizuri hizo elimu. Na wajiepushe na fikra za haya makundi ambayo yanakusudia kuharibu miji na kuondoa umoja wa miji kuhudumia mipango ya maadui, ALLAH ahifadhi miji yetu na miji ya waislamu na awaongoze vijana wetu katika yale yenye hernia apande katika nyoyo zao mapenzi ya nchi zao, hakika ALLAH ni msikivu na mwenye kuwa karibu mno na waja wake.

PROFESA: ABDUL FATTAH ABDUL GHINAA AL AWAARY

MKUU WA KITIVO CHA USUL DDIIN CAIRO – CHUO CHA AL AZHAR

MJUMBE WA TAASISI YA KIMATAIFA YA WAHITIMU WA CHUO CHA AL AZHAR

اظهر المزيد

مقالات ذات صلة

اترك تعليقاً

لن يتم نشر عنوان بريدك الإلكتروني. الحقول الإلزامية مشار إليها بـ *

زر الذهاب إلى الأعلى